At-Tawba 9:96
التوبةيَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا۟ عَنْهُمْ ۖ فَإِن تَرْضَوْا۟ عَنْهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْفَـٰسِقِينَ
Wanawaapia ili muwe radhi nao. Lakini hata mkiwa radhi nao nyiye, basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi na kaumu wavukao mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanakuapieni ili muwe radhi nao. Basi hata mkiwa radhi nao nyiye, Mwenyezi Mungu hawi radhi na watu wapotofu. [96]
[96] Wanakuapieni kwa tamaa ya kutaka muwe radhi nao. Hata mkakhadaika kwa viapo vyao na mkawaridhia, radhi zenu nyinyi peke yenu hazitowafaa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amekasirika nao kwa upotovu wao na uasi wao kuipinga Dini!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanawaapia nyinyi, enyi Waumini, wanafiki hawa kwa urongo ili mridhike nao. Basi mkiridhika nao, kwa kuwa hamjui urongo wao, hakika Allah Mtukufu Haridhiki na hawa wala wengineo kati ya wale walioendelea na uasi na kutoka nje ya utiifu wa Allah Mtukufu na Mtume Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net