Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 95

At-Tawba 9:95

التوبة

سَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمْ إِذَا ٱنقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا۟ عَنْهُمْ ۖ فَأَعْرِضُوا۟ عَنْهُمْ ۖ إِنَّهُمْ رِجْسٌ ۖ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Maana

Watawaapia kwa Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najisi, na makazi yao ni Jahannam, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu mtakapo rudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najsi, na makaazi yao ni Jahannamu, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyachuma. [95]

[95] Watakuapieni kwa Mwenyezi Mungu pale mtapo rejea kwao, kwamba wao wanasema kweli katika kutoa udhuru wao, ili muwaridhie na kwa hivyo waghafilike na vitendo vyao. Basi msiwakubalie kwa lengo lao hilo. Bali watengeni na muwachukie, kwani wao wako daraja ya mwisho kabisa ya ukhabithi wa roho na ukafiri. Na mwisho wao ni Jahannamu, kuwa ndio adabu yao kwa madhambi na maasi walio yatenda!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mtakaporejea kwao kutoka vitani, wanafiki watawaapia nyinyi kwa Allah Mtukufu, wakitoa udhuru hali ya kuwa ni warongo, ili muwaache bila kuwauliza. Basi jiepusheni nao na muwape mgongo kwa kuwadharau, kwani wao ni wachafu wa ndani. Na mahali pao pa kushukia kesho Akhera ni Moto wa Jahanamu, ukiwa ni malipo ya yale waliokuwa wakiyatenda ya madhambi na makosa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net