Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 80

At-Tawba 9:80

التوبة

ٱسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ

Maana

Waombee msamaha au usiwaombee msamaha. Hata ukiwaombea msamaha mara sabini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Waombee msamaha au usiwaombee. Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotofu. [80]

[80] Haitofaa kitu kuwaitikia baadhi yao na ukawaombea maghfira kwa Mwenyezi Mungu. Ewe Nabii! Ukiwaombea msamaha au ukitowaombea, hata ukiwaombea mara ngapi, Mwenyezi Mungu hatowasamehe! Kwa sababu kwa hawa hapana matarajio ya msamaha wala maghfira maadamu wanaendelea na ukafiri wao. Na watu hawa wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wanao kwenda kinyume naye, wakamuasi, na wakenda kinyume na kumuasi Mtume wake, na wakaiasi Sharia yake na Dini yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waombee msamaha hao wanafiki, ewe Mtume, au usiwaombee msamaha, Allah Mtukufu Hatawasamehe, namna yatakayokuwa mengi na kukaririka maombi yako kutaka wasamehewe, kwa kuwa wao wamemkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake. Na Allah Mtukufu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Hawaafikii kwenye uongofu wale waliotoka nje ya utiifu Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net