At-Tawba 9:79
التوبةٱلَّذِينَ يَلْمِزُونَ ٱلْمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ فِى ٱلصَّدَقَـٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ ۙ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Wale wanaowabeua Waumini wanaotoa sadaka nyingi na wasio na cha kutoa ila kiasi cha juhudi yao, hivyo wanawafanyia masikhara. Mwenyezi Mungu atawakejeli wao! Nao wana adhabu chungu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale wanao wabeuwa Waumini wanao toa sadaka nyingi na wasio nacho cha kutoa ila kadri ya juhudi yao, basi huwakejeli. Mwenyezi Mungu atawakejeli wao! Nao watapata adhabu chungu! [79]
[79] Na katika ila zao hawa wanaafiki pamoja na ubakhili wao ni kuwa wao huwakejeli Waumini wenye nafasi kwa vile kusabilia mali yao kwa wanao hitajia, na huwafanyia maskhara wale wenye nafasi ndogo wanao toa sadaka juu ya kuwa wenyewe walicho nacho ni kidogo. Mwenyezi Mungu kesha walipa kwa hizo kejeli zao kwa kuwakashifu wakatambulikana fedheha zao, wakawa wao ndio kichekesho cha watu wote. Na kesho Akhera adhabu yao itakuwa kali.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na pamoja na ubahili wa wanafiki, wale wanaotoa sadaka hawavuki salama na kero lao. Pindi wale matajiri wakitoa sadaka ya mali mengi, wanawatia dowa na kuwatuhumu kuwa wanajionesha. Na pindi mafukara wakitoa sadaka kulingana na uwezo wao, wanawafanyia shere na kusema kwa njia ya kuwachezea, «Sadaka yao hii itawafaa nini?» Basi Allah Mtukufu Anawafanyia shere wanafiki hawa. Na wao watakuwa na adhabu kali iumizayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net