At-Tawba 9:78
التوبةأَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَىٰهُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ عَلَّـٰمُ ٱلْغُيُوبِ
Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua sana ya ghaibu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua sana ya ghaibu? [78]
[78] Vipi wanajitia ujinga na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema? Hapana chochote wanacho dhamiria kisirisiri katika kuvunja ahadi kinacho fichikana kwake. Wala wanacho kinong'ona kwa uficho katika kuitia kombo Dini na kuwapangia njama Waislamu. Naye, aliye tukuka shani yake, ni Mjuzi mno hapitikiwi na kitu chochote..
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hawakujua wanafiki hawa kwamba Allah Mtukufu Anayajua wanayoyaficha ndani ya nafsi zao na yale wanayoyazungumza kwenye mabaraza yao ya vitimbi na njama na kwamba Allah Mtukufu ni Mjuzi sana wa yaliyofichika yote? Basi Atawalipa kwa matendo yao ambayo Amewahifadhia na kuwadhibitia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net