Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 77

At-Tawba 9:77

التوبة

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِى قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُۥ بِمَآ أَخْلَفُوا۟ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا۟ يَكْذِبُونَ

Maana

Basi akawafuatisha unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakapokutana naye, kwa sababu ya kuwa walimvunjia Mwenyezi Mungu yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi akawalipa unaafiki kuutia nyoyoni mwao mpaka Siku watapo kutana naye, kwa sababu ya kuwa walimkhalifu Mwenyezi Mungu katika yale waliyo muahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uwongo. [77]

[77] Matokeo ya ubakhili wao ni kujaa unaafiki katika nyoyo zao mpaka watakapo kufa na wakakutana na Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya kuvunja ahadi zao na uwongo wao katika viapo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ikawa malipo ya mambo waliyoyafanya na mwisho wao ni kwamba aliwaongezea unafiki juu ya unafiki wao, hawataweza kujisafisha nao mpaka Siku ya kuhesabiwa. Hayo ni kwa sababu ya kwenda kwao kinyume na ahadi walioitoa juu ya nafsi zao na kwa sababu ya unafiki wao na urongo wao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net