At-Tawba 9:76
التوبةفَلَمَّآ ءَاتَىٰهُم مِّن فَضْلِهِۦ بَخِلُوا۟ بِهِۦ وَتَوَلَّوا۟ وَّهُم مُّعْرِضُونَ
Basi alipowapa katika fadhila yake, wakaifanyia ubahili na wakageuka hali ya kuwa wamepeana mgongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Alipo wapa katika fadhila yake wakaifanyia ubakhili na wakageuka, na huku wakipuuza. [76]
[76] Mwenyezi Mungu akiwaitikia na akawapa kwa fadhila yake, wanafanya ubakhili. Hawatoi kitu, wala hawatimizi ahadi, na huiacha kheri wakiipuuza na wakimpuuza Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Alipowapa Allah Mtukufu kutokana na hisani yake, walifanya ubakhili kutoa sadaka na kutumia mali katika wema, na waligeuka nyuma hali ya kuupa mgongo Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net