Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 75

At-Tawba 9:75

التوبة

وَمِنْهُم مَّنْ عَـٰهَدَ ٱللَّهَ لَئِنْ ءَاتَىٰنَا مِن فَضْلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ

Maana

Na miongoni mwao kuwa wale waliomuahidi Mwenyezi Mungu kwamba: Akitupa katika fadhila yake, hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika waliotengenea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwao wapo walio muahidi Mwenyezi Mungu kwa kusema: Akitupa katika fadhila yake hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika watendao mema. [75]

[75] Katika wanaafiki wapo ambao humuapia na kumuahidi Mwenyezi Mungu kuwa akiwapa mali na akawatajirisha kwa fadhila yake, basi watatoa sadaka na watakuwa wenye vitendo vyema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa mafukara wa wanafiki, kuna wanaojipa ahadi ya mkazo wenyewe kwamba lau Allah Mtukufu Atampa mali, atayatolea sadaka, atafanya vile watu wema wanafanya katika mali yao na atafuata njia ya wema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net