At-Tawba 9:81
التوبةفَرِحَ ٱلْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَـٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓا۟ أَن يُجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُوا۟ لَا تَنفِرُوا۟ فِى ٱلْحَرِّ ۗ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا ۚ لَّوْ كَانُوا۟ يَفْقَهُونَ
Walifurahi walioachwa nyuma kwa kule kukaa kwao nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wakachukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakasema: Msitoke kwenda katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto kubwa zaidi, laiti wangelikuwa wanafahamu!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walifurahi walio achwa nyuma kwa kule kubakia kwao nyuma na kumuacha Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walichukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao, na wakasema: Msitoke nje katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto zaidi, laiti wangeli fahamu! [81]
[81] Hakika wanaafiki walibaki nyuma wasitoke pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenda kuwakaabili maadui, na wakafurahi kubakia Madina baada ya kutoka Nabii, na kukhalifu amri yake ya kwenda kwenye Jihadi. Walichukia kutumia mali yao na kujitolea roho zao kwa ajili ya Jihadi kulinyanyua Neno la Mwenyezi Mungu na kuinusuru Dini yake. Wakawa wao wakiwavunja moyo wengineo, na wakiwashawishi wabaki nyuma pamoja nao, na wakiwatisha wasende vitani katika joto kama hilo! Ewe Mtume! Waambie hawa: Kama nyinyi mna akili mtakumbuka kuwa vukuto la Moto wa Jahannamu ni kali zaidi na lina shida zaidi kuliko hili mnalo likhofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Walifurahi wale waliojiweka nyuma wasimfuate Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kujikalia Madina wakienda kinyume na Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na walichukia kupigana jihadi pamoja na Yeye kwa mali zao na nafsi Zao katika njia ya Allah Mtukufu na waliambiana wao kwa wao, «Msitoke katika kipindi cha joto.» Waambie, ewe Mtume, «Moto wa Jahanamu una joto zaidi,» lau wao wanalijua hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net