At-Tawba 9:82
التوبةفَلْيَضْحَكُوا۟ قَلِيلًا وَلْيَبْكُوا۟ كَثِيرًا جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Basi na wacheke kidogo, na walie sana. Hayo ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi nawacheke kidogo; watalia sana. Hayo ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyachuma. [82]
[82] Basi nawacheke kufurahia kutokwenda vitani na kuwakejeli Waumini. Kwani kicheko chao muda wake ni mfupi; kitakwisha yatakapo kwisha maisha yao hapa duniani. Tena kitafuata kilio kikubwa kisicho kuwa na mwisho cha huko Akhera. Hayo ni malipo yao kwa madhambi waliyo yafanya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi na wacheke hao wanafiki waliojiweka nyuma wasimfuate Mtume wa Allah Mtukufu katika vita vya Tabûk, kidogo katika uhai wao wa kilimwengu wenye kumalizika, na walie sana katika Moto wa Jahanamu, ukiwa ni malipo ya yale ambayo walikuwa wakiyachuma duniani ya unafiki na ukafiri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net