Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 83

At-Tawba 9:83

التوبة

فَإِن رَّجَعَكَ ٱللَّهُ إِلَىٰ طَآئِفَةٍ مِّنْهُمْ فَٱسْتَـْٔذَنُوكَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا۟ مَعِىَ أَبَدًا وَلَن تُقَـٰتِلُوا۟ مَعِىَ عَدُوًّا ۖ إِنَّكُمْ رَضِيتُم بِٱلْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَٱقْعُدُوا۟ مَعَ ٱلْخَـٰلِفِينَ

Maana

Basi Mwenyezi Mungu akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na wakakutaka idhini ya kutoka - basi sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala hamtapigana na adui pamoja nami. Hakika nyinyi mliridhia kusalia nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao waliosalia nyuma.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi Mwenyezi Mungu akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na wakakutaka idhini ya kutoka - sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala hamtapigana na adui pamoja nami. Nyinyi mliridhia kukaa nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao watakao bakia nyuma. [83]

[83] Ukirejea kutoka vitani wakawa baadhi ya hawa wanaafiki walio kataa kwenda vitani wakakutaka ruhusa watoke nawe kwenda Jihadi katika vita vingine, basi wewe usiwakubalie, na waambie: Hamtokwenda nami katika vita vyo vyote, wala hamtoshirikiana nami katika kupigana kokote na adui. Kwani kukaa kwenu nyuma msitoke pale mara ya kwanza hakukuwa na udhuru wowote unao faa, wala haikutokea toba yoyote ya kustahiki msamaha! Basi kaeni kama mlivyo ridhia kukaa pamoja na wazee na wakongwe na wanawake na watoto wadogo walio bakia nyuma.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi Akikurudisha Allah Mtukufu, ewe Mtume, kutoka kwenye vita ulivyopigana ukaja kwenye kundi la wanafiki waliothibiti juu ya unafiki, na wakakutaka ruhusa watoke na wewe kwenye vita vingine baada ya vita vya Tabûk, waambie, «Hamtatoka pamoja na mimi kabisa kwenye vita vyovyote, na hamtapigana pamoja na mimi na adui yoyote. Nyinyi mumeridhika kukaa mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na wale waliojiweka nyuma wakaacha kupigana jihadi pamoja na Mtume (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie)».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net