Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 6

At-Tawba 9:6

التوبة

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ٱسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَـٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُۥ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ

Maana

Na ikiwa yeyote miongoni mwa washirikina atakuomba ulinzi, basi mpe ulinzi ili apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe mahali pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni kaumu wasiojua kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu. [6]

[6] Ewe Mtume! Mmoja wapo katika washirikina ulio amrishwa uwapige vita, akikutaka amani ili apate kusikia wito wako, basi mpe amani mpaka asikie maneno ya Mwenyezi Mungu. Akiingia katika Uislamu basi huyo ni mwenzenu. Na akitoingia mpeleke mpaka afike pahala pa amani kwake. Na haya ya kumpa ulinzi na amani mwenye kuomba ili asikie maneno ya Mwenyezi Mungu ni kwa sababu ya ule ujinga wake wa kutoujua Uislamu ulio kwisha dhihiri, na ile hamu yake ya kutaka kuujua.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi yoyote, miongoni mwa washirikina ambao damu zao na mali zao zimehalalishwa, akiomba kuingia kwenye himaya yako, ewe Mtume, na akataka amani, basi mkubalie maombi yake ili apate kuisikia Qur’ani tukufu na auone uongofu wake, kisha mrudishe alikotoka akiwa kwenye usalama. Hilo ni kwa sababu ya kumsimamishia hoja, kwa kuwa Makafiri hawaujui uhakika wa Uislamu, kwani huenda wakauchagua pindi ujinga wao ukiwaondokea.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net