Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 5

At-Tawba 9:5

التوبة

فَإِذَا ٱنسَلَخَ ٱلْأَشْهُرُ ٱلْحُرُمُ فَٱقْتُلُوا۟ ٱلْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَٱحْصُرُوهُمْ وَٱقْعُدُوا۟ لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ ۚ فَإِن تَابُوا۟ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَخَلُّوا۟ سَبِيلَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na ikiisha miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni na wazingireni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni njia yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikisha miezi mitukufu basi wauweni washirikina popote mwakutapo, na washikeni na wazungukeni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [5]

[5] Ukimalizika muda wa amani, yaani miezi mine, basi wauweni washirikina walio vunja ahadi katika kila pahala. Na watieni nguvuni, wazungukeni kwa kuwafungia njia, na wavizieni katika kila njia. Wakitubu wakaacha ukafiri wao, na wakafuata hukumu za Uislamu, kwa kushika Swala, na kutoa Zaka, basi nyinyi hamna sababu ya kuwashambulia, kwa kuwa wamekwisha ingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa Kusamehe kwa anaye tubu, na Mwenye rehema kunjufu kwa waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi pindi itakapomalizika miezi minne, ambayo ndani yake mliwapa amani washirikina, basi tangazeni vita juu ya maadui wa Allah Mtukufu popote walipo, na muwalenge kwa kuwazingira kwenye vituo vyao na muwavizie kwenye njia zao. Na iwapo watarudi nyuma kuacha ukafiri wao, wakaingia kwenye Uislamu na wakajilazimisha na sheria zake za kusimamisha Swala na kutoa Zaka, basi waacheni, kwani wameshakuwa ndugu zenu katika Uislamu. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuwasamehe waliotubia na wakarudi nyuma, ni Mwenye huruma kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net