At-Tawba 9:7
التوبةكَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ رَسُولِهِۦٓ إِلَّا ٱلَّذِينَ عَـٰهَدتُّمْ عِندَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ۖ فَمَا ٱسْتَقَـٰمُوا۟ لَكُمْ فَٱسْتَقِيمُوا۟ لَهُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ
Vipi washirikina watakuwa na agano kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake, isipokuwa wale mliofanya agano nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu watawawia wanyoofu, basi nanyi pia wawieni wanyoofu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Itakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake, ila wale mlio ahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu . [7]
[7] Itakuwaje hawa washirikina, wanao vunja ahadi mara kwa mara, wawe na ahadi ya kuhishimiwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake? Basi msichukue ahadi zao, ila wale katika kabila za Kiarabu mlio ahadiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu, na kisha wakasimama sawa kwenye ahadi yao. Basi nanyi simameni sawa juu ya ahadi yenu maadamu wao wamesimama sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kumt'ii Yeye na wenye kutimiza ahadi zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haitakikani kwa washirikina wawe na makubaliano, mbele ya Allah Mtukufu na Mtume Wake, isipokuwa wale mliofanya makubaliano nao kwenye msikiti wa Ḥarãm katika mapatano ya Hudaibiyah. Basi wakiendelea kutekeleza makubaliano yenu, na nyinyi endeleeni na wao kama hivyo. Hakika Allah Mtukufu Anawapenda wenye kumuogopa Allah Mtukufu, wenye kutekeleza ahadi zao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net