Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 8

At-Tawba 9:8

التوبة

كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا۟ عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا۟ فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ يُرْضُونَكُم بِأَفْوَٰهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَـٰسِقُونَ

Maana

Vipi, na wakiwa na ushindi dhidi yenu, hawachungi kwenu udugu wala ahadi. Wanawafurahisha kwa midomo yao tu, lakini nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu. [8]

[8] Vipi nyinyi mtalinda ahadi zao nao ni watu ambao wakikuwezeni wanawasaidia maadui zenu dhidi yenu? Hawataacha fursa ya kukumalizeni bila ya kujali ujamaa (udugu) wala mapatano. Na watu hao hukudanganyeni kwa maneno yao yaliyo pakwa asali, na nyoyo zao zimekunja kwa kukuchukieni. Na wengi wao wametokana na Haki, ni wenye kuvunja ahadi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tabia ya Makafiri ni kujilazimisha na makubaliano iwapo ushindi uko kwa wengine wasiokuwa wao. Lakini wakijihisi kuwa wana nguvu juu ya Waumini, basi wao hawachungi ujamaa wala makubaliano. Basi msidanganyike na vile wanavyowafanyia wawapo na hofu na nyinyi. Kwani wao wanawaambia maneno kwa ndimi zao ili mridhike na wao, lakini nyoyo zao zinakataa hilo. Na wengi wao ni wenye kuupiga vita Uislamu, ni wenye kuvunja ahadi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net