Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 58

At-Tawba 9:58

التوبة

وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِى ٱلصَّدَقَـٰتِ فَإِنْ أُعْطُوا۟ مِنْهَا رَضُوا۟ وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا۟ مِنْهَآ إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ

Maana

Na miongoni mwao kuna yule anayekusengenya kuhusiana na sadaka. Kwa hivyo wakipewa kwayo, wanaridhika. Na wasipopewa kwayo, tazama, wanakasirika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwao wapo wanao kusengenya katika kugawa sadaka. Wanapo pewa wao huridhika. Na wakito pewa hukasirika. [58]

[58] Na baadhi ya hawa wanaafiki wanakusema kwa ubaya, na wanakutia ila katika ugawaji wa sadaka na ngawira. Hawana ila uroho wa makombo ya kidunia tu. Ukiwapa wakitakacho wanakuwa radhi nawe kwa utendayo. Na kama hukuwapa ndio wao ni wepesi wa kukuletea maudhi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa wanafiki, kuna wale wanaokutia dowa katika kugawanya sadaka: wapatapo fungu wanaridhika na wananyamaza, na wasipobahatika kupata fungu wanakukasirikia na kukuumbua.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net