At-Tawba
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِى ٱلصَّدَقَـٰتِ فَإِنْ أُعْطُوا۟ مِنْهَا رَضُوا۟ وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا۟ مِنْهَآ إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ 58
{58} Yaani, miongoni mwa wanafiki hawa wapo wanaokushutumu katika kugawa sadaka na kukukosoa kwa ajili yake. Na kukosoa kwao katika hilo si kwa nia sahihi wala kwa maoni yanayostahili; bali makusudio yao ni kwamba wapewe kwayo. "Kwa hivyo wakipewa kwayo, wanaridhika. lakini wasipopewa, tazama, wanakasirika." Na hali hii haimfailii mja, kwamba iwe radhi yake na ghadhabu yake inafuatana na matamanio yake ya kidunia na makusudio yake maovu. Bali linalomfailia ni kwamba yawe [matamanio yake yanafuatana na] radhi za Mola wake Mlezi. Kama alivyosema Nabii- rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, - “Hataamini mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake yanafuata yale niliyokuja nayo.”