Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 57

At-Tawba 9:57

التوبة

لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَـًٔا أَوْ مَغَـٰرَٰتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا۟ إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ

Maana

Lau kama watapata pa kukimbilia au mapango au mahali pa kuingia, basi hakika wangeligeuka kwenda huko huku wanakimbia mbio zisizozuilika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lau kama wangeli pata pa kukimbilia au mapango au pahala pa kuingia basi wangeli fyatuka mbio kuelekea huko. [57]

[57] Wao hali wanakudhikini na wanachukia kuingiana nanyi, lau wangeli pata ngome, au mapango milimani, au mashimo chini ya ardhi wakaingia humo, basi wangeli yakimbilia mbio!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau wanafiki hawa wangepata mahala pa usalama na ngome ya kuwahifadhi, au pango kwenye jabali litakalowapa makao au handaki ndani ya ardhi itakaowaokoa na nyinyi, basi wangalikwenda huko mbiombio.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net