At-Tawba 9:56
التوبةوَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَـٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni katika nyinyi, wala wao si katika nyinyi. Lakini wao ni kaumu wanaoogopa mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni katika nyinyi, wala wao si katika nyinyi. Lakini ni watu wanao ogopa. [56]
[56] Na hawa wanaafiki hukuapieni kiapo cha uwongo, enyi jamaa Waumini, kwamba wao ni Waumini kama nyinyi. Na hakika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu. Lakini hao ni watu madhaifu na woga, na hayo ndiyo yanayo wapelekea kufanya unaafiki wao, na daima kuwa na khofu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanawaapia wanafiki hawa, enyi Waumini, kwa urongo na ubatili, kwamba wao ni katika nyinyi, wala wao kamwe si katika nyinyi. Lakini wao ni watu waoga, wanaapa kwa kujikinga na nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net