Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 55

At-Tawba 9:55

التوبة

فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَٰلُهُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَـٰفِرُونَ

Maana

Basi zisikufurahishe mali zao wala wana wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwazo katika maisha ya dunia hii, na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yasikufurahishe mali yao wala wana wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwayo hapa duniani, na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri. [55]

[55] Wala usifurahie na moyo wako ukavutika kwa unavyo waona wanaafiki wana mali na wana. Kwani Mwenyezi Mungu hakuwapa hayo ila wapate kuyahangaikia hayo kwa taabu na mashaka wayalinde katika maisha ya duniani, bila ya kupata malipwa yake. Yawakumbe mauti nao wamo katika ukafiri wao, waadhibiwe kwa sababu yake Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Zisikushangaze, ewe Nabii, mali za wanafiki hawa wala watoto wao. Hakika Allah Mtukufu Anataka kuwaadhibu kwa hizo hapa ulimwenguni, kwa tabu ya kuzipata na kwa mikasa inayozifikia kwa kuwa yatokeapo hayo hawatarajii malipo mema kwa Allah Mtukufu, na zitoke nafsi zao wapate kufa juu ya kumkanusha Allah Mtukufu na Mtume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net