At-Tawba 9:54
التوبةوَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَـٰتُهُمْ إِلَّآ أَنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأْتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَـٰرِهُونَ
Na hawakuzuiliwa kukubaliwa kutoa kwao isipokuwa kwa kuwa walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala isipokuwa huku ni wavivu, wala hawatoi isipokuwa nao wamechukia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hawakuzuiliwa kukubaliwa michango yao ila kwa kuwa walimkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala ila kwa uvivu, wala hawatoi michango ila nao wamechukia. [54]
[54] Wala Mwenyezi Mungu hakukataza visipokelewe wanavyo vitoa ila kwa kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na ukafiri, kukataa, kunavunja a'mali zote. Na vile kwa kuwa wao hawaswali kwa namna walio amrishwa; kwani wao huswali bila ya kuiamini Swala, ila wanafanya kama ni kuficha unaafiki wao. Wala wao hawatoi kitu isipo kuwa na huku wanachukia huko kutoa ndani ya nyoyo zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na sababu ya kutokubaliwa wanavyovitoa ni kwamba wao wameficha ukanushaji wao Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, na ukataaji wao ukweli wa Mtume Wake Muhammad (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kwamba wao hawaendi kuswali isipokuwa huku wanaona uzito, na kwamba hawatoi mali yao isipokuwa huku wao ni wenye kuchukia hilo. Wao hawana matarajio ya kupata malipo ya faradhi hizi wala hawaogopi mateso kwa kuziacha kwa ukafiri wao walionao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net