Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 53

At-Tawba 9:53

التوبة

قُلْ أَنفِقُوا۟ طَوْعًا أَوْ كَرْهًا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمْ ۖ إِنَّكُمْ كُنتُمْ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ

Maana

Sema: Toeni kwa kupenda au kwa kuchukia. Kamwe hakitakubaliwa kutoka kwenu. Kwani hakika nyinyi mmekuwa kaumu wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Toeni mkipenda msipende. Hakitopokelewa kitu kwenu, kwani nyinyi ni watu wapotovu. [53]

[53] Ewe Mtume! Waambie hao wanaafiki wanao taka kuficha unaafiki wao kwa kutoa michango ya mali kwa ajili ya Jihadi na mengineyo: Toeni mtakacho, kwa khiari au kwa nguvu; Mwenyezi Mungu havikubali vitendo vyenu vilivyo kwisha haribiwa na unaafiki wenu! Kwani nyinyi daima ni wenye kuiasi Dini ya Mwenyezi Mungu, wenye kuipinga amri yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Nabii, kuwaambia wanafiki, «Toeni mali zenu vile mtakavyo na namna mtakavyo, kwa hiari yenu au kwa kulazimishwa, Allah Mtukufu hatavikubali kutoka kwenu mnavyovitoa, kwa kuwa nyinyi ni watu mliotoka kwenye dini ya Allah Mtukufu na utiifu Kwake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net