Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 52

At-Tawba 9:52

التوبة

قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَآ إِلَّآ إِحْدَى ٱلْحُسْنَيَيْنِ ۖ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ ٱللَّهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِۦٓ أَوْ بِأَيْدِينَا ۖ فَتَرَبَّصُوٓا۟ إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ

Maana

Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipokuwa moja katika mazuri mawili? Na sisi tunawatazamia kuwa Mwenyezi Mungu atawasibu kwa adhabu kutoka kwake, au kwa mikono yetu. Basi tazamieni, nasi hakika tunatazamia pamoja nanyi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipo kuwa moja katika mema mawili? Na sisi tunakutazamieni kuwa Mwenyezi Mungu akufikishieni adhabu itokayo kwake, au kutokana na mikono yetu. Basi ngojeni, nasi tunangoja pamoja nanyi. [52]

[52] Ewe Mtume! Waambie hao: Nyinyi msitaraji yatatutufikia sisi ila moja ya mema mawili, ama tushinde na tupate ngawira, au tufe mashahidi katika Njia ya Mwenyezi Mungu na tuingie Peponi kesho Akhera. Na sisi tunakutarajieni ikufikieni adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu ikuangamizeni; au akuadhibuni kwa udhalili kutokana na mikono yetu. Basi ingojeeni amri ya Mwenyezi Mungu; na sisi pia tunaingoja amri yake pamoja nanyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Nabii, «Kwani kuna mnachokitazamia kwetu isipokuwa tufe mashahidi au tuwashinde? Na sisi tunatazamia kwenu kwamba Allah Mtukufu Atawapatia mateso ya haraka yanayotoka Kwake yawaangamize, au yanayotokana na mikono yetu tuwaue. Basi ngojeeni, na sisi tunalingojea, pamoja na nyinyi, lile ambalo Allah Mtukufu ni Mwenye kulifanya kwa kila kundi kati yetu na nyinyi».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net