At-Tawba 9:51
التوبةقُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوْلَىٰنَا ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ
Sema: Halitusibu isipokuwa yale aliyotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na kwa Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Halitusibu ila alilo tuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu! [51]
[51] Waambie ewe Mtume: Hayatupati ya kheri wala ya shari katika hii dunia yetu, ila aliyo tukadiria Mwenyezi Mungu. Kwani sisi turadhi na hukumu ya Mwenyezi Mungu. Hatujitapi kwa kheri, wala hatuingiwi na dukuduku la roho kwa kufikiwa na shari. Hakika Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kuyatawala mambo yetu yote, na juu yake Yeye tu ndio Waumini wa kweli wanategemea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Nabii, uwaambie hao wanaovunja moyo kwa kujitoa, kwa kuwakemea na kuwaumbua, «Hakuna litakalotupata isipokuwa lile Alilolipitisha Allah Mtukufu juu yetu na Aliloliandika katika al-Lawḥ al-Maḥfûẓ (Ubao Uliohifadhiwa). Yeye Ndiye Mwenye kutupa ushindi juu ya maadui wetu.» Na kwa Allah Mtukufu, Peke Yake, na wajitegemeze wale wanaomuamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net