At-Tawba 9:50
التوبةإِن تُصِبْكَ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ ۖ وَإِن تُصِبْكَ مُصِيبَةٌ يَقُولُوا۟ قَدْ أَخَذْنَآ أَمْرَنَا مِن قَبْلُ وَيَتَوَلَّوا۟ وَّهُمْ فَرِحُونَ
Likikupata zuri, linawawia baya. Na ukikusibu msiba, wanasema: 'Sisi hakika tuliangalia mambo yetu vizuri tangu zamani.' Na wanageuka kwenda zao hali ya kuwa wamefurahi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ukikupata wema unawachukiza, na ukikusibu msiba, wao husema: Sisi tuliangalia mambo yetu vizuri tangu kwanza. Na hugeuka kwenda zao nao wamefurahi. [50]
[50] Hawa wanaafiki hawakutakii wewe Mtume na Masahaba zako ila mambo ya karaha tu. Wanaona uchungu mkipata kheri yoyote, ikiwa ya ushindi au ngawira; na wanafurahi mkisibiwa na shari, kama kujeruhiwa au kuuwawa! Na yakikupateni hayo wao husema kwa kufurahia msiba wenu: Sisi tulichukua hadhari yetu, kwa kubaki nyuma tusitoke kwenda kwenye Jihadi. Na huenda zao nao wamefurahi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Unapofikiwa na furaha na ngawira, wanafiki wanasikitika, na unapopatwa na kero la kushindwa au matatizo, wanasema, «Sisi ni wenye busara na uhodari wa kupanga, tulijipangia kwa maslahi yetu kubakia nyuma na kutomfuata Muhammad.» Na hapo wanaondoka hali ya kuwa na furaha kwa waliyoyafanya na kwa mabaya yaliyokufika.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net