At-Tawba 9:49
التوبةوَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ٱئْذَن لِّى وَلَا تَفْتِنِّىٓ ۚ أَلَا فِى ٱلْفِتْنَةِ سَقَطُوا۟ ۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌۢ بِٱلْكَـٰفِرِينَ
Na miongoni mwao wapo wanaosema: 'Niruhusu wala usinitie majaribuni.' Kwa yakini wao hivyo wamekwishatumbukia katika majaribu. Na hakika Jahannam imewazingira makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na miongoni mwao wapo wanao sema: Niruhusu wala usinitie katika fitina. Kwa yakini wao hivyo wamekwisha tumbukia katika fitina. Na hakika Jahannamu imewazunguka. [49]
[49] Na baadhi ya wanaafiki walikuwa wakimwambia Mtume: Tupe ruhusa tukae tusende kwenye Jihadi, wala usitutie kwenye shida na dhiki. Na wao kwa hakika kwa msimamo huo wamekwisha jitia wenyewe katika maasia, kumuasi Mwenyezi Mungu. Na hakika Siku ya Akhera Moto wa Jahannamu utawazunguka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa wanafiki hawa, kuna wale wanaoomba ruhusa ya kubaki wasiende kwenye jihadi na wanasema, «Usiniingize kwenye mtihani utakaonifikia, katika hali ya kutoka, wa fitina ya kuvutiwa na wanawake.» Hakika wanafiki hawa wameanguka kwenye fitina kubwa ya unafiki. Na kwa hakika, Moto wa jahanamu ni wenye kuwazunguka wanaomkanusha Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho; hakuna atakayeponyoka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net