Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 59

At-Tawba 9:59

التوبة

وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا۟ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَقَالُوا۟ حَسْبُنَا ٱللَّهُ سَيُؤْتِينَا ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ وَرَسُولُهُۥٓ إِنَّآ إِلَى ٱللَّهِ رَٰغِبُونَ

Maana

Na lau kuwa waliridhia kile alichowapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosheleza, Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila yake, na pia Mtume wake; hakika sisi ni wenye kumtaka Mwenyezi Mungu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na laiti wao wangeli ridhia kile alicho wapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosheleza, Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila yake - na pia Mtume wake; hakika sisi ni wenye kumtaka Mwenyezi Mungu! [59]

[59] Na lau kuwa hao wanaafiki wanao kusema kwa vibaya katika ugawaji wa sadaka na ngawira wangeli ridhia wanacho gaiwa na Mwenyezi Mungu, nacho ndicho anacho wapa Mtume wake, na zikatua nafsi zao - ijapo kuwa ni kitu kidogo - na wakasema: Hukumu ya Mwenyezi Mungu imetutosheleza, na Mwenyezi Mungu ataturuzuku kutokana na fadhila yake, na Mtume wake atakuja tupa zaidi kuliko alicho tupa mara hii, na sisi tunataka ut'iifu wa Mwenyezi Mungu na fadhila zake na ihsani zake.. lau wangeli fanya hayo ingeli kuwa kheri kwao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau hawa wanaokutia dowa katika ugawaji wa sadaka wangeridhika na kile ambacho Allah Mtukufu na Mtume Wake waliwagawia na wakasema, «Allah Mtukufu Ndiye Anayetutosha. Allah Mtukufu Atatupa kutokana na nyongeza Zake, na Mtume Wake atatupa kutokana na kile Allah Mtukufu Alichompa. Sisi tuna hamu Allah Mtukufu Atukunjulie na atutajirishe tusihitajie sadaka wala tusichukue sadaka za watu.» Lau wangefanya hivyo, ingalikuwa bora na yenye manufaa zaidi kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net