At-Tawba 9:44
التوبةلَا يَسْتَـْٔذِنُكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ أَن يُجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلْمُتَّقِينَ
Hawakuombi ruhusa wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho ili wafanye Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawatakuomba ruhusa wale wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wasende kupigana Jihadi kwa mali yao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua wachamngu. [44]
[44] Sio mwendo wa Waumini wa kweli wanao muamini Mwenyezi Mungu na Hisabu ya Siku ya Mwisho waje kukutaka ruhusa ya kuto kwenda kuwania Jihadi kwa mali na nafsi, au kuwa wao wabaki nyuma wakuache wewe. Kwa sababu ukweli wa Imani yao unawapendekezesha Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua ukweli wa niya za Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Si katika misimamo ya wanaomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na Siku ya Mwisho kukutaka ruhusa, ewe Nabii, ya kusalia nyuma kwa kutoshiriki kwenye jihadi katika njia ya Allah Mtukufu kwa nafsi na mali. Hiyo ni misimamo ya wanafiki tu. Na Allah Mtukufu Anamjua Anayemuogopa Yeye na kumcha kwa kuzitekeleza faradhi Zake na kujitenga na Makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net