Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 45

At-Tawba 9:45

التوبة

إِنَّمَا يَسْتَـْٔذِنُكَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَٱرْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِى رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ

Maana

Hakika wanakuomba ruhusa tu wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zikatia shaka. Basi hao wanasitasita katika shaka yao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wasio muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na nyoyo zao zikatia shaka, hao tu ndio wanao kutaka ruhusa. Basi hao wanataradadi katika shaka zao. [45]

[45] Wanao kutaka ruhusa ni wale wasio muamini Mwenyezi Mungu kwa Imani ya kweli, wala hawaamini Hisabu yake ya Siku ya Mwisho. Kwa sababu nyoyo zao daima zimo katika shaka na wasiwasi. Nao wanaishi katika hali ya ubabaishi. Na watakuja yapata malipo ya hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika wanaoomba ruhusa ya kusalia nyuma kutoenda kwenye jihadi ni wale ambao hawamuamini Allah Mtukufu wala Siku ya Mwisho wala hawafanyi mema, na nyoyo zao zimekuwa na shaka kuhusu usahihi wa uliyokuja nayo, ewe Nabii, ya Uislamu na sheria zake. Wao wako kwenye shaka yao wanashangaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net