At-Tawba 9:46
التوبةوَلَوْ أَرَادُوا۟ ٱلْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا۟ لَهُۥ عُدَّةً وَلَـٰكِن كَرِهَ ٱللَّهُ ٱنۢبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ ٱقْعُدُوا۟ مَعَ ٱلْقَـٰعِدِينَ
Na wangelitaka kweli kutoka, basi bila ya shaka wangeliliandalia hilo maandalizi ya sawasawa. Lakini Mwenyezi Mungu alichukia kutoka kwao, kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ingeli kuwa kweli walitaka kutoka bila ya shaka wangeli jiandalia maandalio, lakini Mwenyezi Mungu kachukia kutoka kwao, na kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanao kaa! [46]
[46] Na kama kweli hawa wanaafiki walikuwa na niya ya kwenda kwenye Jihadi pamoja na Mtume, wangeli jitayarisha kwa vita na wakajiandalia. Lakini Mwenyezi Mungu Mwenyewe alichukia huko kutoka kwao, kwa kuwa akijua lau wangeli toka nanyi basi wangeli kuwa dhidi yenu si wenzenu. Basi akawatia uzito wasitoke kwa vile nyoyo zao zilivyo jaa unaafiki! Na msemaji wao akasema: Kaeni pamoja na wale wanao kaa wenye udhuru!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau wanafiki wangetaka kutoka pamoja na wewe, ewe Nabii, kwenye jihadi, basi wangalijiandaa kwa matayarisho ya vyakula na vipando. Lakini Allah Mtukufu Amechukia kutoka kwao, ndipo ikawa ni uzito kwao kutoka, kwa mapitisho na Makadirio Yake, ingawa kisheria Amewaamrisha, na wakaambiwa, «Bakieni nyuma pamoja na waliokaa miongoni mwa wagonjwa, madhaifu, wanawake na watoto».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net