At-Tawba 9:47
التوبةلَوْ خَرَجُوا۟ فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا۟ خِلَـٰلَكُمْ يَبْغُونَكُمُ ٱلْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّـٰعُونَ لَهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّـٰلِمِينَ
Lau wangelitoka kati yenu, wasingeliwazidisha isipokuwa mchafuko, na wangetangatanga kati yenu wakiwatakia fitina. Na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza sana. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhaalimu. [47]
[47] Na pindi wangeli toka pamoja nanyi wasinge kuzidishieni nguvu zozote. Lakini wao wangeeneza wasiwasi na kuzidisha fitna, na wakaieneza kati yenu. Na miongoni mwenu wapo wasio jua uovu wa niya zao, na huenda pengine wangeli khadaika na maneno yao, na wakazisikiliza fitna zao. Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema hao wanaafiki, wanao jidhulumu nafsi zao kwa ule uharibifu wanao udhamiria.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lau wanafiki wangalitoka pamoja na nyinyi, enyi Waumini, kwenye jihadi, wangalieneza mgongano katika safu zenu, ubaya na uharibifu, na wanagalikimbilia kueneza fitina na chuki baina yenu, kwa lengo la kutaka kuwafitini kwa kuwazorotesha msipigane jihadi katika njia ya Allah Mtukufu. Na katika nyinyi, enyi Waumini, kuna wapelelezi wa makafiri, wanazisikia habari zenu na wanazipeleka kwao. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi mno wa wanafiki walio madhalimu na Atawalipa kwa hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net