Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 43

At-Tawba 9:43

التوبة

عَفَا ٱللَّهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُوا۟ وَتَعْلَمَ ٱلْكَـٰذِبِينَ

Maana

Mwenyezi Mungu amekusamehe! Kwa nini ukawapa ruhusa kabla ya kukubainikia wale wanaosema ukweli, na ukawajua waongo?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu amekusamehe! Kwa nini ukawapa ruhusa kabla ya kubainikia kwako wanao sema kweli, na ukawajua waongo? [43]

[43] Mwenyezi Mungu amekusamehe, ewe Mtume, kwa kuwaruhusu hawa wanaafiki wabaki nyuma wasende kwenye Jihadi kabla ya kuwa haijabainika kwako ukajua kwamba udhuru wao ni wa kweli, na kuwajua walio waongo kati yao katika madai yao kuwa wanaamini, na kuwa ati wana udhuru za kweli..

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Amekusamehe, ewe Nabii, kwa yale yaliyotokea kwako, ya kuliacha lililo bora zaidi na la ukamilifu zaidi, nayo ni yale ya kuwaruhusu wanafiki kukaa wasiende kwenye jihadi. Ni kwa nini uwaruhusu hawa wakae wasiende vitani, usingojee mpaka wakufunukie waziwazi wale waliosema kweli katika kutaja nyudhuru zao na uwajue warongo miongoni mwao katika hilo?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net