At-Tawba 9:42
التوبةلَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّٱتَّبَعُوكَ وَلَـٰكِنۢ بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ ٱلشُّقَّةُ ۚ وَسَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَوِ ٱسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ
Lau ingelikuwa ipo faida ya papo kwa hapo, na safari fupi, basi hakika wangelikufuata. Lakini waliona kwamba ni mbali na kuna ugumu. Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu: 'Tungeliweza, basi bila ya shaka tungelitoka pamoja nanyi.' Wanaziangamiza nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika hao ni waongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau ingeli kuwa ipo faida ya papo kwa papo, na safari yenyewe ni fupi, wangeli kufuata. Lakini wameona ni mbali na kuna mashaka. Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu: Tungeli weza bila ya shaka tungeli toka pamoja nanyi. Wanaziangamiza nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika hao ni waongo. [42]
[42] Qur'ani inawasusuika wanaafiki kwa kubakia nyuma wakaacha kumfuata Mtume katika Jihadi. Ikasema: Ingeli kuwa walicho itiwa hawa wanaafiki ni pato la kidunia lilio jepesi kulipata, au ingeli kuwa safari yenyewe ya kwendea ni nyepesi, wangeli kufuata, ewe Mtume. Lakini wanaona safari hii ina mashaka! Na watakuapia kwamba lau wangeli weza wangeli toka nawe! Na kwa unaafiki huu na uwongo wanajihilikisha nafsi zao. Na hali haimfichikii Mwenyezi Mungu. Yeye anaujua uwongo wao na atawalipa malipo yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, uliotukuka utukufu Wake, Ameliumbua kundi la wanafiki waliomtaka ruhusa Mtume wa Allah Mtukufu (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ya kusalia nyuma na kutoenda kwenye vita vya Tabûk, kwa kueleza kwamba lau kutoka kwao kungekua ni kwa kufuata ngawira ya karibu iliyo nyepesi kuipata, wangekufuata. Lakini walipoitwa kwenda kupigana na Warumi pembezoni mwa miji ya Shãm katika kipindi cha joto, walitiana uvivu na wakajiweka nyuma. Na watatoa nyudhuru za kusalia kwao nyuma na kuacha kutoka wakiapa kwa Allah Mtukufu kwamba wao hawaliwezi hilo; wanaziangamiza nafsi zao kwa urongo na unafiki, na hali kwamba Allah Mtukufu yuwajua kuwa wao ni warongo katika zile nyudhuru zao wanazozitoa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net