Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 41

At-Tawba 9:41

التوبة

ٱنفِرُوا۟ خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Maana

Tokeni muende mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hayo ni heri kwenu ikiwa mnajua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua. [41]

[41] Enyi Waumini! Akinadi mwenye kunadi kuwa kuna Jihadi, basi itikieni wito huo, mkiwa mmoja mmoja au kwa makundi. Kila mmoja kwa kadri ya uwezo wake, na hali mna uchangamfu kwa nguvu na salama na silaha. Na muwanie Jihadi kwa mali na nafsi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kulitukuza Neno la Mwenyezi Mungu. Katika hayo upo utukufu na kheri kwenu, ikiwa nyinyi ni watu wenye ujuzi ulio baraabara na mnaijua Haki. Na katika maana yaliyo kusudiwa hapa ni: kuwa nendeni mmepanda au kwa miguu, mna silaha nyepesi na nyengine nzito. Na hivi ni katika mbinu maarufu za kisasa. Silaha nyepesi kama panga ni za kuuwana na askari, na silaha nzito ni za kubomoa ngome za maadui.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tokeni, enyi Waumini, kwenda kwenye jihadi katika njia ya Allah Mtukufu, vijana kwa wazee, katika uzito na wepesi, vyovyote mtakavyokuwa, mtoe mali zenu katika njia ya Allah Mtukufu na mpigane kwa mikono yenu ili kulitangaza neno la Allah Mtukufu. Kutoka huko na kupigana huko ni bora kwenu katika hali zenu za sasa na za baadaye kuliko kuwa wazito, kuacha kutoa na kujikalisha nyuma. Basi iwapo nyinyi ni miongoni mwa walio na ujuzi wa ubora wa jihadi na thawabu zake mbele ya Allah Mtukufu, fanyeni mliyoamrishwa na muitikie wito wa Allah Mtukufu na Mtume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net