Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sura ya 9

At-Tawba

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 44

لَا يَسْتَـْٔذِنُكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ أَن يُجَـٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلْمُتَّقِينَ 44

{44} Kisha akajulisha kwamba wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho hawaombi ruhusa ya kuacha jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Kwa sababu matamanio yale waliyo nayo juu ya heri na imani yanawafanya kwenda katika jihadi bila ya kuhimizwa juu ya hilo na mhimizaji yeyote, na zaidi kwamba waombe ruhusa ya kuiacha bila ya udhuru. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema wachamungu." Basi atawalipa kwa yale waliyoyafanya ya kumcha yeye. Na katika kujua kwake wachamungu ni kwamba alijulisha kwamba katika alama zao ni kwamba hawaombi ruhusa ya kuacha jihadi.