At-Tawba 9:16
التوبةأَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا۟ وَلَمَّا يَعْلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَـٰهَدُوا۟ مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَا رَسُولِهِۦ وَلَا ٱلْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ
Je, mlidhani kuwa mtaachwa tu, na Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliopigana Jihadi miongoni mwenu, na wala hawakumfanya yeyote mwendani wao isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je, mlidhani kuwa mtaachwa tu, bila ya Mwenyezi Mungu kuwajuulisha wale walio pigana Jihadi kati yenu, na wala hawakumfanya mwendani wao isipo kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. [16]
[16] Enyi Waumini! Msidhani kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuacheni hivi hivi bila ya kukutieni mtihanini kwa Jihadi na mfano wa hayo. Ndio mwendo wake Mwenyezi Mungu kufanya mitihani, upate dhihiri ujuzi wake kwa wale kati yenu wanao pigana Jihadi, wenye ikhlasi (yaani nyoyo safi), na wala hawawafanyi marafiki, wendani na walinzi, isipo kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenzao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema vitendo vyenu vyote, na atakulipeni kwavyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni katika mipango ya Allah Mtukufu kuwajaribu waja Wake. Basi msidhani, enyi mkusanyiko wa Waumini, kwamba MwenyeziMungu Atawaacha bila ya mtihani ili Apate kuwajua, ujuzi uliyofunuka wazi kwa viumbe, waja Wake ambao wamemtakasia Mola wao katika jihadi yao na hawakuwafanya wasiokuwa Allah Mtukufu na Mtume Wake na Waumini kuwa ni washauri na marafiki. Na Allah Mtukufu ni Mtambuzi wa vitendo vyenu vyote na Atawalipa kwa vitendo hivyo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net