At-Tawba 9:17
التوبةمَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا۟ مَسَـٰجِدَ ٱللَّهِ شَـٰهِدِينَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِم بِٱلْكُفْرِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ وَفِى ٱلنَّارِ هُمْ خَـٰلِدُونَ
Haikuwa kwa washirikina kwamba waiimarishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa wanazishuhudia nafsi zao wenyewe ukafiri. Hao matendo yao yaliharibika, na katika Moto wao watadumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Haiwi kuwa makafiri ndio waamirishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali wanajishuhudishia wenyewe ukafiri. Hao ndio ambao vitendo vyao vimeharibika, na katika Moto watadumu. [17]
[17] Hawawi washirikina ndio wenye kufaa kuamirisha Misikiti ya Mwenyezi Mungu, na hali wao wangali kuendelea na ukafiri wao, na wanautangaza khasa! Vitendo vyao washirikina havitiwi hisabuni, wala hawatolipwa thawabu kwavyo! Wao ni wenye kudumu Motoni Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Si katika mambo ya washirikina kuziamirisha Nyumba za Allah Mtukufu huku wao wanautangaza ukafiri wao wa kumkanusha Allah Mtukufu na wanamfanya kuwa Ana washirika. Washirikina hawa, Siku ya Kiyama, vitendo vyao vyote vitaharibika na mwisho wao ni kukaa milele Motoni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net