Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 18

At-Tawba 9:18

التوبة

إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَـٰجِدَ ٱللَّهِ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا ٱللَّهَ ۖ فَعَسَىٰٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَن يَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُهْتَدِينَ

Maana

Hakika anayeimarisha tu misikiti ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akasimamisha Sala, na akatoa Zaka, na wala hakumnyenyekea isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Swala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu. [18]

[18] Lakini wanao amirisha Misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja peke yake, na wakasadiki kuwapo kufufuliwa na kulipwa, na wakatimiza Swala kama itakikanavyo, na wakatoa Zaka ya mali yao, na wala hawamwogopi ila Mwenyezi Mungu peke yake. Na hao ndio wanao tarajiwa kuwa mbele ya Mwenyezi Mungu waongofu wa kufuata Njia Iliyo Nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hawawi na hamu ya kujishughulisha na Nyumba za Allah Mtukufu na kuziamirisha. isipokuwa wale ambao wanamuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho, wanasimamisha Swala, wanatoa Zaka na hawaogopi, kwa ajili ya Allah Mtukufu, lawama ya yoyote mwenye kulaumu. Hawa waamirishaji ndio waongofu wa njia ya haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net