Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 19

At-Tawba 9:19

التوبة

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ ٱلْحَآجِّ وَعِمَارَةَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ كَمَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَجَـٰهَدَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ لَا يَسْتَوُۥنَ عِندَ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuimarisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuamirisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. [19]

[19] Haifalii kuwafanya washirikina wanao wanywesha maji Mahujaji, na wakauamirisha Msikiti Mtakatifu (wa Makka), katika cheo kama cha wanao muamini Mwenyezi Mungu Mmoja, na wakasadiki kufufuliwa na kulipwa kwa wayatendayo, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu..Hao si makamu mamoja mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kwenye Njia ya kheri watu ambao wameshikilia kujidhulumu wenyewe kwa ukafiri wao, na wakawadhulumu wengineo kwa maudhi yasio kwisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mnayafanya, enyi watu, yale mnayoyasimamia ya kuwanywesha mahujaji na kuuamirisha msikiti wa Ḥarãm ni kama Imani ya aliyemuamini Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu? Haziwi sawa hali za Waumini na hali za makafiri mbele ya Allah Mtukufu, kwani Allah Mtukufu halikubali tendo lolote bila ya Imani. Na Allah Mtukufu hawaelekezi watu wanaozidhulumu nafsi zao kwa ukafiri kwenye mambo mema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net