At-Tawba 9:20
التوبةٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهَاجَرُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ ٱللَّهِ ۚ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ
Wale walioamini, na wakahama, na wakafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao wana daraja kubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofuzu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale walio amini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufuzu. [20]
[20] Wale walio sadiki kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, na wakauhama mji wa ukafiri kuendea mji wa Uislamu, na wakavumilia mashaka ya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa kutoa mali yao na roho zao, hao wana cheo kikubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, kuliko wengineo wasio na sifa hizi. Na hawa ndio wenye kufuzu, kuzipata thawabu za Mwenyezi Mungu na ukarimu wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wale waliomuamini Allah Mtukufu, wakaiacha Nyumba ya ukafiri wakielekea kwenye Nyumba ya Uislamu na wakatoa mali zao na nafsi zao katika jihadi ili kulikuza neno la Allah Mtukufu. Hawa wana daraja kubwa mno kwa Allah Mtukufu, na wao ndio wenye kufaulu kuzipata radhi Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net