Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 21

At-Tawba 9:21

التوبة

يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَٰنٍ وَجَنَّـٰتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ

Maana

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo wana neema za kudumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo watapata neema za kudumu. [21]

[21] Na hao Mwenyezi Mungu Mtukufu anawabashiria rehema kunjufu itakayo waenea, na atawakhusisha radhi zake, na hayo ndiyo malipo makuu. Na Siku ya Kiyama atawatia katika Mabustani, na humo watapata neema zenye kuthibiti na kudumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Waumini hawa waliohama wana habari njema kutoka kwa Mola wao za rehema kunjufu na radhi ambayo hapatakuwa na hasira baada yake; na mwisho wao ni kwenda kwenye mabustani ya Pepo ya milele na neema zisizokoma.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net