At-Tawba 9:22
التوبةخَـٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجْرٌ عَظِيمٌ
Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Watadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa. [22]
[22] Na wao watadumu huko Peponi hawatoki. Na hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa, na thawabu nyingi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hali ya kukaa kwenye mabustani hayo ya Pepo milele. Na hayo ni malipo ya yale waliyoyatanguliza ya utiifu na vitendo vyema katika maisha yao ya ulimwenguni. Hakika Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ana malipo makubwa kwa aliyeamini na akafanya mema kwa kuzifuata amri Zake na kuyaepuka Makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net