Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 23

At-Tawba 9:23

التوبة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوٓا۟ ءَابَآءَكُمْ وَإِخْوَٰنَكُمْ أَوْلِيَآءَ إِنِ ٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْكُفْرَ عَلَى ٱلْإِيمَـٰنِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa marafiki walinzi wenu ikiwa wanaupendelea ukafiri kuliko Imani. Na mwenye kuwafanya marafiki walinzi miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi vyenu ikiwa wanastahabu ukafiri kuliko Imani. Na katika nyinyi atakaye wafanya hao ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhaalimu. [23]

[23] Enyi Waumini! Msiwafanye baba zenu, na watoto wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na wake zenu, ndio wasaidizi wenu wa kukunusuruni maadamu wanapenda ukafiri, na wanaufadhilisha kuliko Imani. Na wenye kutaka manusura kwa makafiri, ndio hao walio iwacha Njia Iliyo Nyooka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mmemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata sheria Yake kivitendo, msiwafanye jamaa zenu, miongoni mwa kina baba, watoto na wengineo, kuwa ni marafiki (mnaowategemea) mkawa mnawasambazia siri za Waislamu na mnawataka ushauri katika mambo yenu, iwapo bado wako kwenye ukafiri na kuufanyia uadui Uislamu. Na yoyote atakayewafanya wao kuwa ni marafiki na akawapa mapenzi, atakuwa amemuasi Allah Mtukufu na Ameidhulumu nafsi yake dhuluma kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net