Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 24

At-Tawba 9:24

التوبة

قُلْ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ وَإِخْوَٰنُكُمْ وَأَزْوَٰجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَٰلٌ ٱقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَـٰرَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَـٰكِنُ تَرْضَوْنَهَآ أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٍ فِى سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُوا۟ حَتَّىٰ يَأْتِىَ ٱللَّهُ بِأَمْرِهِۦ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَـٰسِقِينَ

Maana

Sema: Ikiwa baba zenu, na wana wenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mlizozichuma, na biashara mnazohofia kuharibika kwake, na makazi mnayoyaridhia, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu aje na amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu. [24]

[24] Ewe Mtume! Waambie Waumini: Ikiwa baba zenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo khofu zisibwage, na majumba mnayo starehea kuyakaa, mnayapenda zaidi kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume na Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, hata mkaacha kumuunga mkono Mtume, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu akuleteeni hukumu yake na adhabu yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi wenye kutoka kwenye mipaka ya Dini yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia Waumini, Iwapo mtawafanya kina baba, watoto, ndugu, wake na jamaa wa karibu, mali mlizozikusanya, biashara ambazo mnaogopa zisikose soko na majumba yanayopendeza ambayo mumekaa ndani yake, (iwapo mtayafanya hayo) ni bora kuliko kumpenda Allah Mtukufu na Mtume Wake na jihadi katika njia Yake, basi yangojeni mateso ya Allah Mtukufu na adhabu Yake kwenu. Na Allah Mtukufu hawapi taufiki wenye kutoka nje ya utiifu Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net