Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 15

At-Tawba 9:15

التوبة

وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ ۗ وَيَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba ya amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. [15]

[15] Na Mwenyezi Mungu atazijaza nyoyo za Waumini furaha ya kushinda baada ya kuwa na hamu na khofu, na atawaondolea hasira, na Mwenyezi Mungu atapokea toba ya amtakaye kumkubalia katika wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa ujuzi kwa mambo yote ya waja wake, ni Mkuu wa hikima katika anayo waamrisha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Ataziondoa hasira kwenye nyoyo za Waumini. Na yoyote mwenye kutubia, miongoni mwa wajeuri hawa, basi Allah Mtukufu Humkubalia toba amtakaye. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa ujuzi wa ukweli wa toba ya mwenye kutubia, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji Wake mambo, utengenezaji Wake na sheria Zake Alizowaekea waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net