Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 14

At-Tawba 9:14

التوبة

قَـٰتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ ٱللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ

Maana

Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na awanusuru dhidi yao, na aviponye vifua vya kaumu ya Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini, [14]

[14] Enyi Waumini, piganeni nao! Mwenyezi Mungu atawaonjesha adhabu itokayo mikononi mwenu, na atawadhalilisha na atakupeni ushindi juu yao. Na kwa kuwashinda hao, na kuunyanyua utukufu wa Uislamu, Mwenyezi Mungu atayapoza machungu yaliyomo katika vifua vya Waumini, yaliyo fichikana na yaliyo dhihiri, wakati wote walipo kuwa wakipata maudhi ya makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mkusanyiko wa Waumini,piganeni vita na maadui wa Allah Mtukufu, kwani Aliyetukuka na kushinda Atawaadhibu wao kwa mikono yenu na Atawafanya wanyonge kwa kushindwa na kutwezwa, Atawanusuru juu yao, Ataliinua neno Lake, Atavipoza, kwa kushindwa kwao, vifua vyenu ambavyo kwa muda mrefu viliingiwa na sikitiko na kero kutokana na vitimbi vya washirikina hawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net