Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 13

At-Tawba 9:13

التوبة

أَلَا تُقَـٰتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوٓا۟ أَيْمَـٰنَهُمْ وَهَمُّوا۟ بِإِخْرَاجِ ٱلرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ أَتَخْشَوْنَهُمْ ۚ فَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Je, hampigani na kaumu waliovunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumtoa Mtume, nao ndio waliowaanza mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je, hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio walio kuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini. [13]

[13] Enyi Waumini! Kwa nini msikimbilie kwenda vitani kuwapiga vita washirikina walio vunja mapatano yenu mara kwa mara, na wao walikuwa wakijihimu kumfukuza Mtume Makka na kumuuwa, na wao tena ndio walio kuanzeni kukuteseni na kukufanyieni uadui tangu mwanzo? Je, mnawaogopa? Msiwaogope! Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye anaye stahiki nyinyi mumwogope, kama nyinyi ni wakweli katika Imani yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Msiwe kwenye hali ya kutoamua kuhusu kupigana na hawa watu ambao walivunja ahadi zao na wakafanya hima kumtoa Mtume kutoka Makkah, na wao ndio walioanza kuwaudhi hapo mwanzo. Je mnawaogopa? Au mnaogopa kupambana nao vitani? Allah Mtukufu Ndiye Mwenye haki zaidi ya nyinyi kumuogopa, iwapo kweli nyinyi ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net