Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · At-Tawba
Sura ya 9

At-Tawba

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 16

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا۟ وَلَمَّا يَعْلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَـٰهَدُوا۟ مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَا رَسُولِهِۦ وَلَا ٱلْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ 16

{16} Yeye Mtukufu anawaambia waja Wake Waumini baada ya kuwaamuru kupigana jihadi: "Mlidhani kuwa mtaachwa tu" bila ya majaribio na kutahiniwa, na kuamrisha yale ambayo atabainika kwayo mkweli na mwongo, "na Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliopigana Jihadi miongoni mwenu " Yaani, elimu aliyoijua tangu zamani sasa ije kutokea kwelikweli ili yafungamane nayo malipo na adhabu, ndiyo awajue wale wanaofanya jihadi katika njia yake kwa ajili ya kuinua neno lake. "Na wala hawakumfanya yeyote mwendani wao isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe?" Yaani, rafiki mlinzi kutoka kwa makafiri. Bali wanamfanya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini marafiki walinzi, ndiyo Mwenyezi Mungu akaweka sheria ya jihadi ili lifikiwe kusudio hili kubwa. Nalo ni kwamba wapambanuke wakweli ambao hawaegemei isipokuwa upande wa Dini ya Mwenyezi Mungu na kando na waongo ambao wanadai kuwa na imani ilhali wanachukua wendani na walinzi wengine kando na Mwenyezi Mungu, na Mtume Wake na Waumini. "Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda." Yaani, anajua yale yanayofikia mambo yenu na yale yanayotokea, kwa hivyo anawajaribu kwa yale ambayo yanadhihirisha ukweli wa hali yenu, na atawalipa kwa matendo yenu, mema yake na maovu yake.