Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 124

At-Tawba 9:124

التوبة

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَـٰذِهِۦٓ إِيمَـٰنًا ۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَزَادَتْهُمْ إِيمَـٰنًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ

Maana

Na inapokwishateremshwa sura, basi wapo miongoni mwao wasemao: "Ni nani miongoni mwenu sura hii imemzidishia Imani?" Ama wale walioamini, iliwazidishia Imani, nao wanafurahi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na inapo teremshwa Sura wapo miongoni mwao wasemao: Ni nani miongoni mwenu Sura hii imemzidishia Imani? Ama wale walio amini inawazidishia Imani, nao wanafurahi. [124]

[124] Na ikiteremka Sura ya Qur'ani wakaisikia wanaafiki huifanyia maskhara na kuikejeli. Huambizana wao kwa wao: Nani katika nyinyi iliyo mzidisha Imani? Ndio Mwenyezi Mungu anawajibu ya kwamba ipo farka baina ya wanaafiki na Waumini. Ama Waumini ndio wale walio iona Nuru na wakaijua Haki. Hao Aya za Mwenyezi Mungu zimewazidishia Imani, na wao huzifurahia wakati zinapo teremka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi Allah Mtukufu Aiteremshapo sura, miongoni mwa sura za Qur’ani, kwa Mtume Wake, basi kati ya hawa wanafiki kuna wanaosema, kwa kukanusha na kufanya shere, Ni nani wenu ambaye sura hii ilimfanya imani yake, kwa Allah Mtukufu na aya Zake, iongezeke? Basi wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, kule kuteremka sura, kuliwaongezea waoImani kwa kuijua na kuizingatia na kuiamini na kuitumia, na hali wao wanafurahia Imani na yakini Alizowapa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net