Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 123

At-Tawba 9:123

التوبة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قَـٰتِلُوا۟ ٱلَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ ٱلْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا۟ فِيكُمْ غِلْظَةً ۚ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ

Maana

Enyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu miongoni mwa makafiri, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mungu. [123]

[123] Enyi mlio amini! Piganeni na makafiri walio karibu yenu ili wasiwe ndio sababu ya kukutieni khatarini. Na kueni wakali kwao mnapo pigana, wala msiwafanyie upole. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu kwa msaada wake na nusra yake yu pamoja na wanao mcha.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkaifuata sheria Yake kivitendo, anzeni kupigana na walio karibukaribu na Nyumba ya Uislamu, miongoni mwa makafiri, na wakute kutoka kwenu ushupavu na ukali. Na jueni kwamba Allah Mtukufu yuko pamoja na wachamungu kwa msaada Wake na nusura Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net